Wednesday, 10 January 2018

Vitu vya kuzingatia unapo"pimp" gari lako

Uliwahi Kuitazama series ya "Pimp My Ride?"
 Kwenye series hiyo, walikuwa wanachukua gari ya kawaida ya mtu na kuiongezea vifaa kadhaa, kuipaka rangi, kubadilisha siti n.k. ile kuifanya ya kisasa zaidi.
Sasa, sio lazima kumsubiri mtu aje kutengeneza gari yako. kuna njia nyingi za kuiboresha gari yako mwenyewe, kwa gharama nafuu:
1. Ongeza spika
Ukiongeza spika za ziada, muziki utakaopigwa au ukiwa unasikiliza redio, utakuwa una sikiliza kwa ubora zaidi. Pia, ukiwa na rafiki zako, pati itaanzia humo humo ukiwa mnatoka.
2. Badilisha Rangi
Hamna kitu kitakachofany gari yako iwe na muonekano mpya kama kubadilisha rangi yake. Kubadilisha rangi ya gari ina gharama ya juu kidogo ila itaongeza thamani ya gari yako, hasa ukiwa tayari kuiuza.
3. Badilisha Rims Zako au Zipake Rangi
Jinunulie Plasti Dip alafu ziweke kwenye rims zako. Baada ya hapo unaweza kuzipaka rangi nyusi au rangi yoyote ile inayopatikana. Plasti Dip imetengezwa kwa mpira kwa ajili ya kuzipa rims zako muonekano mpya.
Plasti Dip inapatikana kwenye duka ya spea za magari au kwenye gereji.
4. Badilisha kasha ya Steering Wheel
Ujipatia cover ya steering wheel cover, alafu iwe ya ngozi, utakuwa umepachangamsha sehemu ya gari ambayo huwa husahauliwa.
5. Badilisha Kichwa cha Gia
Ukibadilisha kasha la steering, badilisha na kichwa cha gia au ipatie kasha (linalofanana na steering).
Dokezo: Pia, nunua kasha za siti na pamoja na jamvi za kupangusia miguu zinazofanana na gia na steering.
6. Weka Tint
Kwa kuweka tint utakuwa umeipa siri kidogo. Pia, ni nzuri kwa usalama wa vitu ndani ya gari.
7. Taa za Nje
Utaweza kuona vizuri zaidi kwa kuongeza taa za nje. Pia, gari lako litapendeza zaidi.
8. Mfumo wa Usalama / Alam
Hakikisha gari lako lina mfumo wa usalama/alam ya maana yenye uhakika.
9. Weka  Jokofu ya kubeba
Weka Jokofu ndogo ya kubeba kati ya siti za mbele. Hii itakuwezesha kuwa na vinywaji vya baridi kila utakapotaka.
10. Namba za Usajili za kipekee
Jipatie namba za Usajili za kipekee. Sio gharama kubwa na litafanya gari yako iwe yako kiukweli.
Ongeza thamani ya gari yako kwa kuiongezea vifaa na vingine. Utapenda kuiendesha zaidi na zaidi.

Magari matano yanayotumia mafuta kidogo (Economy Fuel) Zaidi


Zaidi ya kuwa bugudha, foleni inaongeza matumizi ya mafuta, hasa kwenye miji ya watu wengi kama Arusha, Mwanza na Dar.
Iwapo, kuwa tabia za kubana matumizi ya mafuta kama kudumisha gari lako, kuzima AC na kuendesha kwa spidi ya kawaida yatasaidia, bora uwe na gari isiyotumia mafuta mengi.
Uzuri wa magari yasiotumia mafuta mengi ni kwamba si lazima yawe ghali. Na tumeziorodhesha hapa.
1. Toyota IST
IST ni gari ambayo wanunuzi wake ndio mara yao ya kwanza kuwa na gari au watu wenye bajeti ya kawaida wanaotaka gari la kila siku ambayo ni rahisi kuidumisha.
Kutegemeana na mwaka na hali yake kwa ujumla, zinaweza zikakugharmia TZS 8m – TZS 12m.
2. Toyota Vitz
Vitz inafanana na IST kwenye utendaji ila ni ndogo zaidi na nafuu zaidi. Ila, injini yake ina nguvu yakutosha.
Kutegemeana na mwaka na hali yake kwa ujumla, zinaweza zikakugharmia TZS 6m – TZS 9m.

3. Toyota Passo
Kwa swala la ubunifu, Passo ni kubwa zaidi ya Vitz ila ikijia kwenye maswala ya utendaji, yanatofautiana kidogo sana. Watu watano wanatosha kwenye gari hii pamoja na mizigo na pia, gari linaweza kutembea 100km kwa lita 7.
Kutegemeana na mwaka na hali yake kwa ujumla, zinaweza zikakugharmia TZS 6m – TZS 8.5m.

4. Nissan March
Ingawa inaonekana ndogo, ndani kuna nafasi ya kutosha kabisa kwa sababu ya jinsi matairi yalipowekwa pamoja na uwezo wa viti vya nyuma kuvunjwa. Pia, udogo wake inaiwezesha kupenya barabarani.
Kutegemeana na mwaka na hali yake kwa ujumla, zinaweza zikakugharmia TZS 4m – TZS 6m.
5. Honda Fit
Ubunifu wa Honda Fir ndio kinachoiwezesha kuwa na matumizi mazuri ya mafuta. Badala ya kuifanya iwe kubwa zaidi, na hivyo kuongeza uzito wake, Honda waliamua kwamba wataongeza nafasi kwa kuweka tenki la mafuta chini ya viti vya mbele na kupandisha viti vya nyuma. Hii imewezesha gara hii kutembea 100km kwa 7.1L.
Kutegemeana na mwaka na hali yake kwa ujumla, zinaweza zikakugharmia TZS 8m – TZS 14
Faida haziishi
Kuwa na gari yenye matumizi mazuri ya mafuta itakupunguzia gharama ya uendeshaji sana! Sasa kwa kuwa una chaguo za magari yasiotumia mafuta mengi, pitia magari yanayouzwa kupitia ZoomTanzania.


Matengenezo Matatu ya Gari Yako Unayopaswa Kujua

Kila mtu mwenye gari hafurahii akiwa barabarani na kutambua kwamba gari haliko sawa. Inakuwa mbaya zaidi ukiwa huna hakika kwamba tatizo ni nini.
Ila, matatizo ya yanayotokea huwa yana husisha vitu vitatu. Na bahati nzuri, huhitaji kuwa mtaalam wa magari kuzitengeneza.
1. Betri Iliyokwisha
Gari yako ikikataa kuwaka, kuna uwezekano mkubwa kwamba betri imekufa. Kuna sababu nyingi ya hii kutokea, zikiwemo:
  • Uliacha taa zikiwaka kwa muda mrefu
  • Nguvu ya betri haiendani na nguvu gari
  • Betri imeingia maji
  • Betri ni ya muda mrefu na imechoka
Licha ya sababu, unaweza kuwasha gari lako kwa muda mdogo kwa kufanya yafuatayo:
  • Tafuta gari lingine
  • Zime magari yote mawili
  • Fungua boneti
  • Angalia betri ilipo
  • Angalia sehemu za kukonekti nyaya
  • Toa nyaya zako za kubusti gari
  • Ambatisha upande mwekundu (positive) kwenye terminal ya positive ya betri. Ambatisha upande nyeusi/bluu (negative) kwenye terminal ya negative ya betri.
  • Washa gari la pili kwa daka 5
  • Washa gari lililo kataa kuwakaka. Ikiwaka, iache kwa daka 5
  • Toa nyaya za kubusti.
  • Endesha gari lako na kama tatizo hii itatokea tena, tembelea duka la betri ili ununue betri mpya.
2. Fyuzi Iliyoungua
Ukikuta kwamba redio, indiketa au kifaa kingine linalotumia umeme haiwaki, kunauwezekano mkubwa kwamba fyuzi imeungua. Bahati nzuri tatizo linaweza kushughulikiwa haraka:
  • Fungua boneti, utakuwa boksi ya fyuzi kwenye bay ya injini au steering wheel. Kama huioni, itafute kwenye mwongozo ya gari.
  • Toa funiko ya boksi ya fyuzi. Utaona namba tofauti na rangi kuonyesha nguvu ya kila fyuzi.
  • Tafuta alafu toa fyuzi iliyoungua
  • Unapaswa kuwa na fyuzi ya akiba kwenye gari lako. Kama huna jaribu yafuatayo:
    • Kutumia fyuzi nyingine ya nguvu hiyohiyo kutoka kwenye sehemu nyinge ya gari (kwa mfano redio), au
    • Iache gari yako mpaka utakapo kwenda gereji au kwenye duka la spea za magari ambapo unaweza kununua fyuzi unayohitaji.
  • Jaribu kuwasha gari yako kuona kama tatizo limetatuliwa.
  • Kama fyuzi ikiungua tena, ipele kwa fundi wako.
3. Pancha:
Gari yako itapata pancha mara moja au nyingine. Bahati nzuri, sio tatizo kubwa na wala haihitaji fundi.
  • Washa taa zako za dharura alafu paki gari lako kwenye eneo yenye usalama.
  • Toa vifaa vifuatayo:
    • Jeki
    • Bisibisi
    • Lug Wrench (ya kufungua tairi)
  • Toa tairi yako ya spea kutoka kwenye buti.
  • Tumia Lug Wrench kufungua gurudumu za tairi yenye pancha
  • Weka jeki chini ya gari alafu anza kuipandisha
  • Fungua tairi
  • Weka tairi ya spea alafu hakikisha unaikaza sana
  • Shusha jeki
  • Tumia lug wrench kukaza gurudumu za matairi zaidi
  • Rudisha kila kitu kwenye gari na endelea na safari yako.
Kuna wauzaji wengi wa matairi mazuri kwa ajili ya aina mbalimbali za magari.
Unaweza!
Kujifunza kuhusu gari yako na namna gani ya kufanya matengenezo madogomadogo ni muhimu sana. Kwanza hakikisha spea zote za magari unazo. Hii itakusaidia kujiamini zaidi barabarani na pia itakuokolea muda na gharama ukipata tatizo lingine ndogo.

Sababu za magari aina ya Toyota kuwa maarufu Tanzania

Hata kipofu anajua kwamba Toyota ina umaarufu kuliko kampuni zote za magari Tanzania. Kwa mujibbu wa Best Selling Cars, 1 kati ya magari 4 inayonunuliwa Tanzania ni Toyota.
Sasa, ni kwa nini Toyota zinapendwa hivi?
1. Gharama Nafuu
Toyota iliyotumika kidogo Japan ni gharama nafuu zaidi ya Ford kutoka marekani (au hata nchini). Pia, serikali ya Tanzania inawaruhusu wauzaji wenyeji kuingiza magari haya kwa gharama za chini zaidi. Kwa, bei yake ya kununua nayo ni chini kulingana na magari mengine.
2. Hazitumii mafuta mengi
Magari madogo ya Toyota yanajulikana kwa kutotumia mafuta mengi. Hata magari yao makubwa mengine (Prado kwa mfano), hayatumii mafuta mengi kukizilinganisha na magari makubwa ya makampuni mengine. Kwa mji kama Dar es Salaam yeneye foleni nying, hii ni muhimu.
3. Upatikanaji wa spea
Kwa kuwa Toyota ni maarufu sana, spea zake zinapatikana kiurahisi zaidi pia, ambayo inapunguza gharama ya utunzaji.
4. Zina wataalam wengi
Kwa kurudia, Toyota ni maarufu sana Tanzania na hivyo, fundi wengi wa magari wana ujuzi wa magari ya Toyota.
Mtu mwenye gari la Volkswagen Polo, kwa mfano, atapata shida sana kutafuta fundi mzuri na pia, matengenezo yatakuwa ya gharama kubwa zaidi.
5. Kuna aina ya gari kwa wote
Swala la kuchagua gari la kununua ikijitokeza, watu wengi wanafikiria aina za Toyota na sio aina za magari. Toyota ina aina nyingi za magari zinazokidhi mahitaji ya watu mbalimbali. Kwa kifupi, mtu yoyote anaweza akaendesha Toyota.
Labda sisi ndio wenye mchango mkubwa nchini kwa umaarufu wa Toyota
Ukweli ni kwamba watanzania wana amua kununua gari kutokana na mapendekezo ya family au marafiki. Kwa kweli, kwa kuwa Toyota ni maarufu kuliko wengine ni rahisi sana kutafuta gari ya kampuni hiyo tu. Ila, kuna faida ya kuangalia magari ya makampuni mengine pia.

Picha na maelezo haya ni kwa msaada wa Zoom Tanzania